BERMUDA TRIANGLE:
Hii ni hadithi yenye ukweli ndani yake inayopatikana katika eneo la Bahari ya Atlantiki ya Kaskazini, ikipakana na kisiwa kinachoitwa Bermuda, Miami, na Puerto Rico.
Ni mahali pekee ambapo siri zote za ulimwengu zimefichwa! Kwa kiswahili tinaita Pembetatu ya Bermuda.
Unajua nini kuhusu Bermuda Triangle? Swali hili lingejibiwa kitaalamu na kwa mifano halisi isiyo na shaka na mkali wa hizi mambo, DUPA MDUPANGE.
Hata hivyo hakijaharibika kitu nitakujuza kuhusu mahali hapa ambapo ni hatari zaidi duniani.
Eneo lipo katika Bahari ya Atlantiki huko Amerika Kaskazini, milki ya Florida, ikiwa na kina cha mita 8380 na eneo linalofunika ni maili 40,000.
Hadi sasa, zaidi ya meli 50 na ndege zaidi ya 20 zilipotea katika eneo hilo na maelfu ya watu kufa kwa kupita ama kufika eneo hilo, lililopakana na Visiwa vya Caribbean upande wa kusini.
Kuhusu ukweli wa mahali hapa pa kushangaza, ni moja ya vitu visivyojulikana zaidi duniani hadi leo na mtu wa kwanza kupaona mahali hapa alikuwa ni Christopher Columbus.
Columbus alipaona mahali hapa alipokuwa akisafiri kuzunguka ulimwengu na akaandika, hihi, “Kutoka mbali mwanga wa ajabu huangaza kutoka angani, na nguvu inayoizunguka huzunguka dira moja kwa moja, Watu wengine huita pembetatu ya Bermuda, Sehemu mpya ya Dunia au, ardhi maalum.”
Pembetatu ya Bermuda ilizipoteza Meli, Ndege na maisha ya wengi kuhitimishwa kwa njia ya ajabu, pakiwa ni mahali pekee duniani ambapo usafiri wa anga na nchi kavu hauwezekani kukauiza eneo hilo, kwani itameza kila kitu.
Hivyo kuhusu mahali hapa pamekuwa chanzo cha maumivu ya kichwa kwa Watafiti wengi na Wanasayansi.
Kiufupi wameshindwa kuchunguza ukweli wa mahali hapa. Lakini baadhi ya wataalam wanakadiria ama kukisia mambo yafuatayo.
1. Kuna wingu kubwa la uwanda wa Sumaku na nguvu ya umeme katika eneo ambalo linaweza kuingiliana na nguvu za ndege na meli.
2. Nguvu zisizojulikana za asili (UFOs) zimekaa hapo.
3. Kimbunga kikubwa zaidi duniani kinaweza kuwa karibu.
4. Kuna mto wa kasi baharini na unavuta ndege na meli na panajulikana kama eneo ambalo kwa maajabu meli na ndege hutoweka tangu karne iliyopita.
Mengi yana maelezo kama vile hitilafu za sumaku, maharamia, kuzamishwa kwa makusudi, vimbunga, amana ya gesi n.k.