Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imekamata kilogramu 1,815 za dawa za kulevya aina ya skanka katika operesheni iliyofanyika Agosti 28, 2024 hadi Septemba 2, 2024 katika maeneo ya Luguruni Mbezi na Magomeni jijini Dar es Salaam ambapo watuhumiwa watano wamekamtwa na dawa hizo.

Akitoa taarifa mbele ya Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam hii leo Septemba 10, 2024, Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo amesema watuhumiwa waliokamatwa wanatambulika kwa majina ya Richard Henry Mwanri (47) ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa Mbezi Makonde wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na Felista Henry Mwanri (70) mkulima na mkazi wa Luguruni Mbezi Wilaya ya Ubungo ambaye ni mmiliki wa nyumba zilipokutwa dawa hizo za kulevya.

Watuhumiwa wengine ni Athumani Koja Mohamed (58) mfanyabiashara na mkazi wa Tanga, Omary Chande Mohamed (32) dereva bajaji na mkazi wa Buza jijini Dar es Salaam na Juma Abdallah Chapa (36) mkazi wa Kiwalani jijini Dar es Salaam.  Aidha, katika operesheni hiyo, gari aina ya Mitsubishi Pajero yenye namba za usajili T 551 CAB na bajaji yenye namba za usajili MC 844 CZV vilikamatwa.

Taifa Stars: Tupo tayari kuwasambaratisha Guinea
Malimwengu: Ukweli kuhusu Jiwe la Mwanamke mjamzito