Chama kikuu cha ushirika – KCU 1990 Limited, kimekabidhi Pikipiki 30 na vishikwambi 30 kwa ma2afisa Ugani wa Wilaya tatu za Mkoani Kagera, ili kuongeza tija katika sekta ya Kilimo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni 133 kwa Wilaya za Bukoba, Missenyi na Muleba hii leo Septemba 10, 2024 Mkuu wa Wilaya Bukoba Erasto Sima amesema lengo ni kuongeza ufanisi katika Kilimo.

Amesema, “nitoe wito kwenu maafisa ugani vifaa hivi tulivyovipata leo vitumike katika malengo yaliyokusudiwa ziwe pikipiki ua vishikwambi.”

Mwenyekiti wa Chama hicho, Res Mashurano amesema vifaa hivyo vitasaidia kukidhi matakwa ya Wakulima ambapo na kuwafikia kwa urahisi.

Kwa upande wao Maofisa Ugani waliozungumza na Dar24 Media akiwemo Godlove Erasto na Heleonora Alexander wamesema hapo mazingira waliyokuwa wakifanyia kazi hayakuwa rafiki.

Vita ya maadili kuanzia Ruvuma, Msigwa atoa maelekezo
Taifa Stars: Tupo tayari kuwasambaratisha Guinea