Afarah Suleiman,  Babati – Manyara.

Mkuu wa Wilaya wa Babati, Emmanuela Kaganda amewapongeza Wananchi wa Mkoa wa Manyara kwa kujitokeza kuboresha taarifa katika Daftari la Kudumu la Wapiga kwenye vituo vilivyopo karibu na makazi yao.

Kaganda ametoa pongzi hizo wakati alipofika kuhusha taarifa zake katika kituo kimoja cha Babati Mjini na kusema hiyo ni fursa ya kikatiba na haki ya msingi kushiriki katika zoezi hilo ambalo linaendelea katika Jimbo la Uchaguzi Mkoani Manyara.

Amesema, “zoezi halichukui muda mrefu hivyo wananchi wanaweza kujitokeza na kujiandikisha kwa muda mfupi kisha kurejea katika majukumu yenu ya kila siku.”

Aidha, Kaganda pia ametoa wito kwa wale wote ambao wamefikisha umri wa miaka 18 kuendela kujitokeza kujiandikisha, ili waweze kushiriki katika uchaguzi wa Mwaka 2025.

Feisal,Mudathir wampigia simu Karia
Yanga kuilipa Azam shilingi milioni 88.5