Mahakama ya Juu ya Kenya, imesitisha kwa muda mkataba wa kukodishwa kuwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta – JKIA wa jijini Nairobi, kwa muda wa miaka 30, kwa kampuni ya India ya Andani Group, kwa lengo la kuupanua.

Mbele ya Mahakama, Chama cha Mawakili – LSK na Shirika la kutetea haki za Binadamu la Kenya Human Rights Commission – KHRC, walisema Kenya inaweza kujipatia dola bilioni 1.85 zinazohitajika kukarabati uwanja huo, bila msaada kutoka nje.

Wamesema, kuchukuliwa kwa hatua hiyo kunatishia ajira za watu na haina faida yoyote kwa walipa kodi wa Kenya, huku Kampuni ya Andani ikiwa haijasema lolote kufuatia hatua hiyo.

Mwezi Agosti, 2024 Muungano wa Wafanyakazi wa uwanja huo ulitishia kuitisha mgomo kwa madai kuwa mkataba huo ungepoteza ajira zao.

Ahmed Ally:Tunakwenda kuwaonyesha ubaya ubwela Al Ahli
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Septemba 11, 2024