Mauricio Pochettino ameteuliwa rasmi kuwa kocha mkuu mpya wa Marekani kufuatia kuondoka kwa Gregg Berhalter.Berhalter alitimuliwa baada ya kushindwa kufanya vyema kwenye michuano ya Copa Amerika iliyofanyika Marekani ambapo kichapo cha kkutoka kwa Panama kiliifanya USA kushindwa kufuzu hatua za robo fainali ya michuano hiyo.
Pochettino aliripotiwa kuchukua mikoba hiyo baada ya kuondoka Chelsea akiitumikia timu hiyo kwa msimu mmoja pekee.
Muajentina huyo – ambaye hapo awali alifurahia miaka mitano ya kuinoa Tottenham, na kuwaongoza hadi fainali ya Ligi ya Mabingwa wa 2018-19 – na msimu wa 2023/24 aliisababishia Chelsea kumaliza nafasi ya sita kwenye Ligi ya Premia
Sasa amekubali kuiongoza Marekani katika Kombe la Dunia la nyumbani mwaka wa 2026, huku wakijiandaa kuandaa michuano hiyo pamoja na majirani Canada na Mexico.
Pochettino aliiambia tovuti ya Soka ya Marekani: “Uamuzi wa kujiunga na Soka ya Marekani haukuwa tu kuhusu soka kwangu; ni kuhusu safari ambayo timu hii na nchi hii ziko.Nguvu, shauku, na njaa ya kufikia kitu cha kihistoria hapa – hayo ndiyo mambo ambayo yalinitia moyo.
“Fursa ya kuiongoza timu ya taifa ya wanaume ya Marekani mbele ya mashabiki ambao wana shauku sawa na wachezaji ni jambo ambalo sikuweza kuacha.Ninaona kikundi cha wachezaji kilichojaa talanta na uwezo, na kwa pamoja, tutaunda kitu maalum ambacho taifa zima linaweza kujivunia.”