Afarah Suleiman, Babati – Manyara.

Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa Manyara, Bahati Haule ametoa wito kwa Wananchi na Mamlaka zinazohusika kutojihusisha na vitendo vya rushwa kipindi cha uchaguzi wa Serikali za mitaa na Uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, ili waweze kupata viongozi bora na watakao waletea maendeleo.

Ameyasema hayo mjini Babati wakati akiwasilisha mada kuhusu kuijua TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Majukumu yake na kutoa wito kwa jamii kutojihusisha na kupokea wala kutoa Rushwa katika kipindi cha Uchaguzi.

Aidha Haule amesema TAKUKURU Mkoani Manyara itamshunghulia mtu yeyote atakayejihusisha na vitendo vya rushwa au ushawishi wowote wenye viashiria vya rushwa.

Serikali yataka miradi iendane na thamani ya fedha
Pochetinno:Tunakwenda kuipa marekani Kombe la Dunia 2026