Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limewakamata Wahamiaji haramu 12, wakiwemo watoto wadogo raia wa Burundi, kwa kosa la kuingia nchini bila kibali.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama, ameeleza kuwa watuhumiwa hao walikamatwa Septemba 4, 2024 katika Kata ya Dakawa, Wilaya ya Mvomero, wakifanya kazi kwenye mashamba ya miwa.

Amewataja waliokamatwa kuwa ni Tusenge Juvenal (25), Nshimumukiza Eloje (20), Nibizi Elia (30), Nduwayo Ally (21), Niyomwungere Jabal (18) na Nimbona Pierre (34).

Wengine ni Ndayishimye Jean (20), Kamaliza Geraridine (28), pamoja na watoto Niyoniziye Sandrine (8), Kezakimana (6), Miburo Malitha (4), na Josefu Nikora (14).

RC Dkt. Batilda awatahadharisha Wananchi Kipindipindu, Mpox
Rais Samia awapa Milioni 30 Serengeti Girls