Boniface Gideon – Tanga.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dkt. Batilda Buriani amewataka wakazi wa Mkoa wa Tanga kuchukua tahadhari ya magonjwa yakuambukiza ikiwemo Homa ya Nyani na kipindupindu huku akiuagiza uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo, kuwa ya mfano kama ilivyokuwa wakati wa janga la Uviko-19.

Dkt Buriani ametoa Rai hiyo hii leo Septemba 11, 2024 alipofanya ziara ya kukagua na kutembelea maendeleo ya miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Hospital hiyo kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma ambapo pia kamati ya usalama ya mkoa ilikabidhi bango linaloonyesha tahadhari za kujikinga na ugonjwa huo.

Amesema, ugonjwa huo ambao kwasasa umesharipotiwa katika nchi za Kenya, Uganda na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ni lazima upewe tahadhari kwani Mkoa wa Tanga upo jirani pamoja na muingiliano wa watu kutoka Kenya, wanaokuja Tanzania katika kwa shughuli mbalimbali za kibinadamu ikiwemo za biashara.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dkt. Batilda Buriani akizungumza na Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo.

“Tuna changamoto ya homa ya nyani ‘Mpox’ tulifikiri katika hospital ya kwqnza kabisa ya mkoa ndio muwe kielelezo sijaona hata mabango mliyoyaweka ya kuonyesha tahadhari ya Empox, sasa hivi kama Empox ipo Kenya ,Uganda, Congo kufika Tanzania sio shida tutaweza tu kuokoka kama tutazingatia masharti ya kujikinga na ugonjwa huu ikiwemo maswala ya kurudi kule tulikofanya wakati wa COVID-19 kuweza kunawa mikono kwa maji tiririka na kutokushikana mikono ili kuepukana na ugonjwa huu,” amesema Dkt. Batilda.

Aidha, amesema kutokana na uwepo wa ugonjwa wa kipindipindu ulioibuka katika Wilaya ya Kilindi na wagonjwa 88 kuripotiwa zilifanyika jitihada za makusudi ikiwemo timu ya wataalam kuweka Kambi na kufanikiwa kupunguza maambukizi hayo huku Serikali ikiendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuhakikisha inaboresha huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama.

“Tuna changamoto ya kipindipindu kinaendelea kuisha na sasa kipo kwenye wilaya yetu ya Kilindi tulikuwa tuna wagonjwa 88 ndani ya wiki moja tuliagiza wataalamu waweke Kambi wahakikishe kwamba kusiyokee mgonjwa mwingine tena na sasa leo (Jana) nimeambiwa amebaki mgonjwa mmoja,” alisema.

Ameongeza kuwa, “hii imetokana na vyanzo vya maji kutokuwa salama wenzetu wa Kilindi wanategemea sana maji ya Kisima na chem chem tunayo miradi mikubwa ya maji ambayo inaendelea kukamilishwa mpaka ikifika mwakani tutakuwa tumefikia asilimia 95 ya miradi iliyokamilika mjini na vijijini itakuwa ni 85.”

Zaidi ya Kilo 13 za Dhahabu zadakwa zikitoroshwa, watatu mbaroni
Wahamiaji haramu 12 wadakwa wakifanya kazi Mashamba ya Miwa