Mwaka 1980, Mtu mmoja aliyefahamika kama Richard, aliwasha Luninga yake na haikupita muda wakati akiangalia moja ya vipindi akamwona mchezaji wa kike kutoka Romania akipokea hundi ya Dola 40,000 baada ya kushinda mashindano ya Tenisi.

Tukio hilo kiuhalisia lilimshtua Richard kwani kiasi hicho cha pesa kilikuwa ni kikubwa zaidi kuupita mshahara wake wa mwaka mzima, hali ambayo ilimsumbua sana na akajiapiza kwamba ni lazima binti zake pia watacheza Tenisi.

Kilichofuata Richard alizima Luninga na akaketi kuandika hati ya kurasa 78 iliyoeleza mpango wa binti zake wawili wachanga kukimbia mji wao wa Compton California, eneo linalojulikana kwa visa vya ujeuri vya majambazi weusi.

Sasa kulikuwa na tatizo pia kwamba Richard alikuwa hajui lolote kuhusu Tenisi, hakuwa na pesa za kuwalipia mabinti zake wafanye mazoezi ya mchezo huo wa gharama kubwa na  cha kushangaza ni kwamba mabinti aliokuwa akitaka waingie kwenye mchezo huo walikuwa bado hawajazaliwa.

Miaka mitano iliyofuata, alikusanya magazeti na kaseti za video zinazohusiana na Tenisi ili kujifundisha kucheza Tenisi na miaka mitano mingine, mpango wa Richard ulifanikiwa kwani tayari alikuwa na racquet ya tenisi mikononi mwa binti zake wawili.

Sasa alikuwa kwanza baba na pia kocha wa wasichana hawa wadogo, kwani sasa alianza kuwafundisha mchezo wa tenisi.

Hata hivyo, kwa kushindwa kumudu mambo ya msingi ya kucheza mchezo huo, Richard alienda kwenye vilabu vya nchi za ndani kukusanya mipira ya Tenisi iliyotumika kutoka kwenye mapipa na kuichukua, ili binti zake wafanye mazoezi na mipira hii iliyotumika kwenye viwanja vya Tenisi vya umma.

 

Richard alikuwa mlinzi kupita kiasi na mwenye nguvu kimwili kama baba, na mara nyingi alipigwa na wanyanyasaji wa magenge mahali hapo alipokuwa akijaribu kuwalinda binti zake dhidi ya kunyanyaswa wakati wa mafunzo ya tenisi.

Kuna wakati aliwahi kujeruhiwa alipokataa kutoka eneo la mazoezi pamoja na binti zake, kipigo hicho kilipelekea kupoteza meno yake kadhaa.

Baada ya tukio hilo Richard aliandika katika shajara yake, “Baada ya leo, historia itamkumbuka mtu asiye na meno kama ukumbusho wa ujasiri.”

Kiufupi Richard ndiye Baba wa Venus Williams na Serena Williams, ambao wameshinda mataji ya Mashindano mengi ya Tenisi na Hawaii kinyonge yaani wana mahela.

DC Hazali: Wananchi waambiwe ukweli kuhusu fedha za Miradi
Dkt. Tulia asisitiza kipaumbele cha Elimu, ajira kwa Vijana