Mkuu wa wilaya ya Hanang’ Mkoa wa Manyara, Almishi Issa Hazali amewataka Viongozi wa Vijiji kuwashirikisha Wananchi kabla na wakati wa ujenzi wa miradi mbalimbali, inayojengwa na Serikali katika maeneo yao, ili kuwapa fursa ya kufutilia maendeleo ya miradi hiyo.

DC Hazali ameyasema hayo katika kijiji cha Majengo kilichopo kata ya Measkron wakati akizungumza na wananchi wa kijiji hicho ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kusikiliza, kutatua kero mbalimbali sanjari na kuhamasisha wananchi kushiriki utekelelezaji wa miradi ya maendeleo na ukusanyaji wa mapato ya ndani.

Amesema, wananchi wanayo haki ya kufahamu kinachoendelea katika vijiji vyao ili kuwapa nguvu ya kushirikiana na serikali hasa kwa kujitolea nguvu kazi pale serikali inapotoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na kulipa mapato ili kuchochea maendeleo.

Ulinzi maudhui ya ndani: Vitabu kutoka nje vikaguliwe - Kamati
Maisha: Serena, Venus Williams walivyomtoa meno baba yao