Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Elimu Utamaduni na Michezo wamegundua kuna tofauti ya viwango vya utekezaji wa miradi ya Taasisi za Umma au za Serikali na viwango vya utekezaji wa miradi ya Halmashauri za Wilaya mkoani Pwani na kutaka uwepo uwiano sawa wa utekezaji wa miradi.

Akitoa maelekezo hayo Wakati wa majumuisho ya ziara ya siku moja ya ukaguzi wa utekezaji wa mradi ya idara ya elimu wilayani Kibaha mkoani Pwani Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Elimu Utamaduni na Michezo, Husna Sekiboko ameutaka Uongozi wa mkoa wa Pwani wahakikishe uwiano sawa katika Utekelezaji wa Miradi ya taasisi za umma na miradi ya halmashauri za wilaya.

Amesema, “tumegundua kuna tofauti kubwa katika utekezaji wa miradi ya taasisi za Wizara na miradi ya halmashauri za wilaya Sasa tunaagiza tunataka viwango sawa na vinavyokubalika vya gharama za utekezaji wa miradi ya taasisi za Wizara na Halmshauri za wilaya.”

“Niliuliza swali dogo tulipokuwa kwenye ukaguzi wa darasa la elimu ya watu wa wazima pale nikaambiwa ni kama milioni 26 mpaka milioni 28 lakini kiasi hicho hicho ndio kina kwenda kwenye utekezaji wa miradi ya ujenzi wa madarasa ya halmashauri zetu Sasa tunataka kuona viwango vya ujenzi wa miradi ya serikali kwenye taasisi zote za umma iwe serikali au miradi ya taasisi za Wizara iwe kwenye viwango vinavyokubalika ubora wake,” aliongeza Husna.

Aidha, akizungumzia vitabu vya kufundishia, Husna imetaka Wizara ya Elimu sayansi na Technologia kukagua vitabu vya kufundishia ili kubaini kama mitaala iliwekwa inazingatia maadili ya kitanzania na kama vinazingatia malengo ya taifa kufikia hatua za maendeleo.

Alisema, vitabu hivyo iatavyokaguliwa na kuhakikiwa vipitishwe kwa kuwekwa muhuri wa kamishina wa Elimu ili kutofautisha na vitabu vingine ambayo sio vya kufundishia darasani.

“Tunataka mahudhui ya vitabu vyote ikaguliwe na kupitiwa kitabu kwa kitabu kuanzia vitabu vya Shule za serikali mpaka vya Shule binafi maana wanaosoma ni watoto wa kitanzania hivi vitabu vya misaada kutoka nje ya nchi kama nchi za India, China hata marekani vikaguliwe na kuhakikiwa mahudhui yake” alisema Mheshimiwa Husna.

Aidha Mwenyekiti wa Kamati huyo aimeka Wizara ya Elimu kuhakikisha vitabu vinavyopelekwa mashuleni kuhakikisha vinagongwa muhuli wa kamishina wa Elimu.

Kwa upande wake Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Pro Adolf Mkenda akiwa Katika Ziara hiyo amewatakia Mtihani Mwema Darasa la Saba ambapo Leo ni Simu ya pili ya mitihani Yao na kuwataka Kufanya mtihani bila udanganyifu wowote.

Ziara hiyo ya Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Elimu Utamaduni na Michezo imetembelea Shule ya Sekondary Shimbo Pamoja na Kituo Cha Elimu ya Watu wazima kinachohusisha wasichana waliokatiza masomo yao na kurejea shuleni.

Amesema hayo baada ya Kufanya Ziara Wilaya ya Kibaha na kutembelea Shule ya Sekondary ya Shimbo na Kituo Cha Elimu ya Watu wazima halmashauri ya Kibaha mji.

Aloyce Kamamba, Mbunge Jimbo la Buyungu Kankoko kigoma ameipongeza Serikali Kwa hatua ya Utekelezaji miradi mbalimbali ikiwamo Elimu ya Watu wazima na Kutoa Ushauri wanafunzi hao Kuwa na Walimu maalum.

Majaliwa: Miradi ya Dola Bilioni 8.65 imesajiliwa ndani ya mwaka
DC Hazali: Wananchi waambiwe ukweli kuhusu fedha za Miradi