Mabao ya Josephat Bada dakika ya 40 na Elvis Rupia yameipeleka Singida Black Stars katika nafasi ya Kwanza ya msimamo wa ligi kuu NBC. Timu hiyo chini ya kocha Patrick Aussems imekuwa na mwanzo mzuri baada ya kucheza mechi tatu na kuvuna alama 9 zinazowaweka kileleni mwa ligi wakifuatiwa na Simba wenye alama 6 katika michezo miwili waliyocheza.
Singida Black Stars walianza vyema ligi kuu NBC kwa msimu wa 2024/25 kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Ken Gold uwanja wa Sokoine Mbeya.ushindi wa bao 1-0 uwanja wa ugenini Kaitaba na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya KMC mchezo uliopigwa uwanja wa Liti Singida.Mchezaji Emanuel Keyekeh aliibuka nyota wa mchezo dhidi ya KMC
Timu hiyo imefunga jumla ya mabao 6 na kufungwa mabao 2 katika mechi 3 walizocheza.
Huu hapa msimamo wa ligi kuu ya NBC