Johansen Buberwa – Kagera.
Hospital na vituo vya Afya maeneo yote Mkoani Kagera wametakiwa kutenga maeneo maalumu ya dharura pindi inapotokea majanga ya moto ili yaweze kutoa usaidizi wakati wa makabiliano.
Akizungumza wakati akitoa mafunzo kwa watumishi wa Afya katika Hospital ya Wilaya ya Bukoba hii leo Septemba 13, 2024, Sajini wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji, Shaban Mussa ambaye pia ni Afisa Habari wa jeshi hilo Mokoani Kagera amesema kwasasa kuna umuhimu mkubwa wa maeneo ya Afya kuwa na kitengo kilichokamalika, ili inapotokea majanga iwe rahisi kusaidia.
Amesema, kuwa na vifaa vya tahadhari vikiwemo vizimia moto kwa watumishi kwa uhalisia kuwa wapo mazingira ya kazi muda wote ni muhimu kwani kuna wagonjwa wanaolazwa hivyo inaweza kutokea majanga ya moto au tetemeko la ardhi na hivyo wawe salama.
Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Bukoba, Dkt. Jovin Stanislaus amelishukuru Jeshi la Zimamoto na uokoaji kwa kuwafikia na kuwapatia elimu ya majanga ya moto inahudumia wagonjwa wa nje 800, Wanawake wanaojifungua kawaida 90 hadi 100 na wanaofanyiwa upasuaji 40 mpaka 45.
Kwa upande wake Innocenta Ngowi Katibu wa Afya Hospitali ya Wilaya Bukoba amesema elimu hiyo waliyo ipata itasaidia kudhibiti endapo moto utatokea.
Naye Shantar Naftar Muheta ambaye ni Mtunza Kumbukumbu Mwandamizi Hospitali hiyo akimuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuwasaidia jengo la kitengo cha dharura pamoja na kuajiri watumishi, ili kusaidia endapo ikitokea majanga waweze kukabiliana nayo.