Mkaguzi Kata ya Ngara Mjini, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Olipa Chitongo amekutana na wahitimu wa Shule ya Msingi Nyabihanga Wilaya ya Ngara Mkoa wa Kagera na kuwapa Elimu na mbinu ya kuepuka vishawishi mara baada ya kuhitimu elimu yao ya Msingi.

Olipa ametoa elimu hiyo kwa wahitimu hao huku akiwataka kutoshawishiwa na watu kwa mahusiano ya kimapenzi kwani watapoteza ndoto zao ikiwa ni pamoja na maendeleo yao kielimu.

Aidha, amewataka kutumia vizuri muda wa kusubili matokeo kwa kujiongezea ujuzi katika kozi za muda mfupi ili ziwataisaidie baada ya kufaulu na kuendelea na masomo yao ya Sekondari.

Sambamba na hayo, Mkaguzi Olipa pia amewaomba Wanafunzi hao kuwa mabalozi wazuri katika kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi, juu ya wahalifu na uhalifu katika maeneo yao.

 

Serikali kuweka unafuu upatikanaji bidhaa Nishati safi ya kupikia
Zimamoto: Hospitali, Vituo vya Afya vitenge maeneo ya dharura