Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka ameonesha kutoridhishwa na ubora wa meza na viti zaidi ya mia mbili kwenye ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya sekondari Vidunda.

DC Shaka amekutana na hali hiyo akiwa kwenye ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kusikiliza changamoto za wananchi ili zipatiwe ufumbuzi.

Kwa mujibu wa viongozi wa Kijiji kata Akiwemo diwani Bwana Godian Makuye amedai kuwa viongozi hao hawajashirikishwa suala la meza hizo kutengenezwa mkoani Dar es Salaam.

 

Amesema wataalam kutoka halmshauri ya Wilaya kilosa ndio walioshauri meza hizo zitengenzwe mkoani Dar es salaam kwa madai kuwa ndio Kuna mafundi wazuri na mbao nzuri

Kufiatia hali hiyo, DC Shaka amesema Serikali itachukua hatua kwa kukuta ujenzi wa.mdarasa na meza hizo upo chini ya kiwango.

BMH waendelea kuimarisha huduma za Afya
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Septemba 14, 2024