Tofauti kati ya masikini na tajiri ni tabia.

Masikini ni nani.

Masikini kwa mujibu wa wakubwa wanasema ni mtu ambaye anatia huruma kwa sababu ni mlemavu, amepatwa na msiba mkubwa, au ana uwezo duni kiuchumi.

Hata hivyo, mara nyingi mtu hutajwa kuwa maskini pale ambapo hana uwezo wa kumudu maisha au kupata mahitaji yake muhimu, yaani makazi mazuri, mavazi mazuri na chakula kizuri.

Mtu maskini wakati mwingine huwa hana uhakika wa kula, uhakika wa kununua mavazi na uhakika wa kupata matibabu pale atakapoumwa.

Tajiri ni yupi.

Hapa hakuna maneno mengi, na ndivyo ilivyo maana ya neno hili ni mtu mwenye wingi wa mali, imetosha.

Tukirudi katika mada ipo hivi …. kiuhalisia Masikini wanatumia pesa nyingi kwenye dhima na ndio maana huwa wanakuwa na maumivu.

Wengi wa watu walio maskini ninaowajua ni wafujaji na wapumbavu (siwatusi nazungumzia uhalisia na sina maana mbaya maana upumbavu ni kisifa).

Wao mara nyingi hununua vitu vingi ambavyo hawahitaji na ni wachache tu kati yao wanaofanya mambo yao kama matajiri tena wakiwa na hofu juu ya kesho yao.

Watu maskini ndiyo ambao wana uwezekano mkubwa wa kufanikiwa baadaye kama wangeheshimu kidogo walichonacho, lakini kwa wengi ipo tofauti.

Masikiji anaweza lala njaa lakini kesho yake akipata 5,000 atataka kila mtu afahamu ana hela, hivyo huanza kumwaga radhi atanunua kila kilicho mbele yake, bila kujali wakati ujao.

Na hapa ndipo pale Wahenga wakaja na ‘michambo’ kama ule wa Masikini akipata Matako hulia mbwata, sema kwenye msemo huu nina wasiwasi kuna masikini waliujadili nao wakarudi na wao wakisema ‘ponda mali kufa kwaja’.

Halafu masikini pia huwa ni jeuri usisikie, wana maneno ya kishujaa na yanayoendelea kuwapa uhai na nguvu ya utafutaji wasiyoipa heshima kimatokeo mpaka leo.

Ipo hivi, kuna wakati niliwahi pewa lift na Mkubwa wangu alikuwa na corolla old model imechoka balaa lakini ipo barabarani, tukiwa tunaenda zetu mjini ikatupita Range rover Vogue, nikaiangalia sana ndugu yangu dereva akanishtukia akasema, “tulia dogo ile na hii zote zinaingia sheli.”

Nilitaka kucheka kwa nguvu lakini kimoyomoyo nikajisemea “ngoja nitulie nisijeshushwa mie,” hata hivyo cheko lilinitoka bila utaratibu pale aliposema eti hata tukitoka wote (ile Vogue na Corolla) Dar – Moro wote tunafika ila tutapishana masaa tu.

Yaani kiukweli masikini ni mashujaa sana we angalia hata Polisi wetu wa usalama Barabarani huwa hawashughuliki na gari za maana zenye majina yake, ila ikipita kirikuu ina mchicha na Nyanya au fuso imebeba Parachichi, itakiona kilichomtoa Kanga manyoya.

Hata mabasi, we angalia basi zilizosoma shule kama Marcopolo, Higer, Scania, Irizer, Yutong nk huwa haziguswi hovyo ila kutana na chombo imetoka Ushetu, Malinyi au Namanyele, yaani ni itawekwa kushoto utadhani imepakia sumu au vilipuzi, kumbe imebeba tu watu wa kipato cha chini na wala haina shida lakini …. acha tu.

Angalia hata tunavyoshughulikia matatizo yetu, waweza kuta kuna msiba umetokea kwenu Kibaha kwa Mathias, wewe unaishi Maili moja lakini kwakuwa huna hela unaweza shitukia unaulizwa tena siku ya pili na jirani yako “we jamaa vip mbona uko hapa na wenzako wanazika kule.”

Kibaya zaidi ukifika msibani umechelewa wameshazika, unabaki kushangaa nao wanakushangaa, ukitizama kuna ndugu yako tajiri katoka Durban yupo pale anamwaga dolari kwa wanafamilia, we mfukoni una “AFUMBILI” na una makosa tayari hujakaa sawa unasikia ‘jombi chukua hii kawanunulie kuni wamama zimeisha’ yaani daah …. inauma.

Masikini tuna roho mbaya tuna hasira hasira kwanza me nishakasirika siandiki tena kuhusu matajiri.

Barabara zinazojengwa zikamilike kwa wakati - Mchengerwa
BMH waendelea kuimarisha huduma za Afya