Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa amefanya kikao kazi na walimu wa shule za Sekondari wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa walimu hao.

Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Wakuu wa Idara na Vitengo, Watendaji wa Kata, Waratibu wa Elimu Kata, Walimu wa Kujitolea na wasomi wazawa wanaojishughulisha na Elimu waliopo katika Halmashauri hiyo ya Wilaya ya Rufiji.

Aidha, Mchengerwa amekagua ujenzi wa barabara za Ikwiriri katika Halmashauri hiyo, ambazo zinajengwa na Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) na kuhimiza zikamilishwe kwa wakati na viwango stahiki.

Mradi heshimu Bahari wazinduliwa Bagamoyo
Maisha: Kausha dogo, wote tunaingia sheli