Kutokana na maisha ya zaidi ya asilimia 70 ya Wananchi wa Wilaya ya Bagamoyo kuunganishwa na bahari ya Hindi yanayotegemea uchumi wa bahari Katika sekta ya utalii, usafirishaji na Uvuvi, Taasisi ya Sea Sense imezindua Mradi wa USAID Heshimu bahari.
Mradi huo unaotekelezwa Wilaya ya Bagamoyo ukiwa na Malengo ya kuimarisha ustahimilivu wa kimazingira na uzalishaji wa Maeneo ya kiikolojia bahari.
Akizungumza Wakati wa ufunguzi wa Mradi wa USAID Heshimu bahari unaotekelezwa Bagamoyo Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Rashid Mchata amewapongeza Sea Sense Kwa Mradi ambao muhimu Kwani utasaidia Kuokoa mazao ya bahari na utaongeza juhudi za Pamoja Katika kutatua Changamoto zinazokabili Mazingira ya bahari.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa sea Sense Gosbert Katunzi amesema rasilimali za bahari zimekuwa zikipungua kwa Kasi kwasababu ya Uvuvi usioendelevu na Uvuvi haramu.
Aidha Meneja wa Mradi USAID Heshimu bahari Kutoka Sea Sense Lydia Mgimwa anaeleza namna Mradi huo ulivyoundwa na utakavyotekelezwa na wadau mbalimbali.
Mradi huu USAID Heshimu bahari utasaidia Wananchi wa Bagamoyo Katika kuboresha Hali ya Maisha Kwa kuondoa umasikini ,utasaidia kuondoa Hali ya umasikini ,na kutoa Elimu juu ya utunzaji wa bahari