Johansen Buberwa – Kagera.
Mkuu wa Wilaya Bukoba Erasto Sima amemkabidhi Mkandarasi wa kampuni ya managing Director Nice Construction & General Suppliers Limeted mkataba wa mradi wa maji wenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 4 utaohudumia kata saba za Wilaya hiyo Mkoani Kagera kwa kipindi cha miezi 18.
Sima ameyasema hayo wakati wa kuwasilisha taarifa ya hali ya upatikanaji wa huduma ya maji ndani ya Manispa hiyo Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (Buwasa) Mkoani Kagera John Sirati katika utiaji sani na makabidhino ya mradi wa nyanda za juu kwa mkandarasi Daniel Lameck wa kampuni ya managing Director Nice Construction & General Suppliers Limeted kata ya Ijuganyondo.
Amesema, Mamlaka hiyo inahudumia kata zote 14 na hali ya upatikanaji wa maji kwa sasa umefikia asilimia 90 na wananchi wanao nufaika na huduma hiyo ni 149,000 chanzo kikuu ni ziwa Victoria ambapo mahitaji ya maji kwa Manispa hiyo ni lita Bilioni 14 na laki tano kwa siku na mamlaka hiyo inazalisha lita bilion 10 na laki tano kwa siku ambapo mradi huo mpya wa nyanda za juu usaidia kuhudumia kata tano na mahitaji yake ni lita million 7 na laki 5 na 57 elfu.
“Kata hizo zitakazo nufaika na mradi mpya ni Rwamishenye,kibeta,kitendaguro,Ijuganyondo na kagondo pamoja kata mbili za Halmashauri ya Bukoba vijiji ni kata za Karabagaine na Katoma ambapo kata hizo bado zinakabiliwa na upungufu wa maji kutona na kata hizo kukua kwa kasi na hali inayopelekea kuwa na matumizi makubwa ya huduma hivyo wanapata kwa mgao kutoka na ujenzi wa chuo kikuu tawi la Dar es Salaam ndani ya kata Karabagaine kuwa na matumizi makubwa,” amesama Meneja Sirati.
Aidha, Sima piq ameipongeza mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Buwasa kwa namna inavyo kuwa inaendelea kutoa huduma kwa wananchi wake na kumtaka mkandarasi aliyesani pamoja na kukabidhiwa mkataba asimamia mradi huo ukamilike kwa wati.