Johansen Buberwa – Kagera 

Serikali ya Wilaya Bukoba, imemkabidhi Mkandarasi wa kampuni ya managing Director Nice Construction & General Suppliers Limeted mkataba wa mradi wa maji wenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 4 utaohudumia kata saba za Wilaya hiyo Mkoani Kagera kwa kipindi cha miezi 18.

Makabidhiano hayo yamefanyika wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya hali ya upatikanaji wa huduma ya maji ndani ya Manispa hiyo, utiaji saini na makabidhiano ya mradi wa nyanda za juu kwa mkandarasi Daniel Lameck wa kampuni ya managing Director Nice Construction & General Suppliers Limeted kata ya Ijuganyondo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (BUWASA) Mkoani Kagera, John Sirati amesema mamlaka hiyo inahudumia kata zote 14 na hali ya upatikanaji wa maji kwa sasa umefikia asilimia 90 na wananchi wanao nufaika na huduma hiyo ni 149,000 chanzo kikuu ni ziwa Victoria.

Amesema, mahitaji ya maji kwa Manispa hiyo ni lita Bilioni 14 na laki tano kwa siku na mamlaka hiyo inazalisha lita bilion 10 na laki tano kwa siku ambapo mradi huo mpya wa nyanda za juu usaidia kuhudumia kata tano na mahitaji yake ni lita million 7 na laki 5 na 57 elfu.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Bukoba, Mjini Wakili Stephano Byabato ameshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupata mradio huo na kumuomba mkandarasi atakayesimamia mradi kuwapatia vijana kipaumbele cha ajira katika meneo yao unapopita mradi wa maji.

Naye Mkuu wa Wilaya Bukoba, Erasto Sima ameipongeza mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Buwasa kwa namna inavyo kuwa inaendelea kutoa huduma kwa wananchi wake na kumtaka mkandarasi aliyesani pamoja na kukabidhiwa mkataba asimamia mradi huo ukamilike kwa wati.

Shaban Robert, King Majuto wapata mgeni Tanga
Wanawake wahimizwa kutumia fursa