Jumla ya Vijiji 12, 333, Mitaa 4,269 na Vitongoji 64, 274 vitashiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika November 27, 2024.

Tangazo hilo limetolewa na Waziri wa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa  Jijini Arusha hii leo Septemba 16, 2024 na kusema orodha hiyo imejumuisha maeneo yaliyokuwa yamefutwa awali kwa mujibu wa tangazo la Serikali ambayo pia yalihusisha Tarafa ya Ngorongoro.

Amesema, “matangazo haya yanajumuisha maeneo yaliyokuwa yamefutwa awali kwa mujibu wa tangazo la Serikali namba 673 na 674 ambayo yalihusisha pia Tarafa ya Ngorongoro, lengo la hatua hii ni kuhakikisha kuwa maeneo haya yanapata uwakilishi mzuri kiutawala pamoja na huduma za kijamii na kiuchumi zinazowiana na mahitaji ya Wananchi.”

Aidha Mchengerwa pia amesisitiza umuhimu wa Wananchi kujitokeza kushiriki katika uchaguzi huo katika kuunda Serikali ya Wananchi kidemokrasia kwa kujiandikisha kwa wingi kwenye daftari la Mpiga kura.

Sheikh Mkuu: Waislam tuache vitendo viovu, tudumishe amani
Uwezekano wa Mvua Mikoa ukanda wa Pwani