Waislamu Nchini, wametakiwa kuendelea kuhubiri amani na kuachana na vitendo viovu vinavyoweza kupelekea uvunjifu wa amani ya Taifa iliyopo.
Rais hiyo, imetolewa na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Alhaji Dkt. Abubakar Zuber Bin Ally Mbwana katika Sherehe za Maulid ya Kitaifa iliyofanyika katika Viwanja vya Kalangalala Mjini Geita.
Amesema “Mtume alikuwa Mtu wa subra, alikuwa Mtu wa pole, alikuwa akifundisha amani, Mungu alimtayarisha akawa ni Mtu wa namna hiyo hakufanya mambo ya kipuuzi hata siku moja.”
Sheikh Mkuu pia ameongeza kuwa, “Mungu ametueleza katika Quran juu ya masuala ya amani ni ajabu Umma huu leo ikawa hawa ndio wanaovunja amani wao ndio wanaoharibu ulimwengu, msilete uharibifu, msieneze uharibifu katika Nchi. Tusisumbuliwe na Watu, kikundi au fikra za baadhi ya Watu kwa makusudio yao.”