Baadhi ya maeneo ya mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Lindi, Mtwara, Pwani ikijumuisha visiwa vya Mafia, Unguja na Pemba yanatarajia kupata mvua nyepesi usiku wa leo.
Taarifa hiyo imetolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini – TMA, huku ikitoa angalizo la mawimbi makubwa yanayofikia mita mbili kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa Pwani ya kaskazini ya Bahari ya Hindi kwa mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani ikijumuisha visiwa vya Mafia, Unguja na Pemba.
Kuhusu uwezekano wa kutokea kwa athari TMA imeeleza kuwa wastani na shughuli zinazoweza kuathirika ni za kiuchumi, uvuvi na usafirishaji wa baharini.
Kwa Mikoa ya Kagera na Geita yenyewe itakuwa na mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua wakati mikoa ya Mara, Shinyanga, Simiyu na Mwanza itashuhudia hali ya mawingu kiasi, ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
Aidha, TMA pia imesema, “Mikoa ya Dodoma, Singida, Kigoma, Tabora na Katavi,Morogoro, Manyara, Arusha na Kilimanjaro, Ruvuma, Rukwa, Mbeya, Njombe, Iringa na Songwe zitashuhudia mawimgu kiasi na vipindi vya jua.”