Death Valley (Bonde la Kifo), ni bonde la jangwa lililopo huko California Mashariki, Kaskazini mwa Jangwa la Mojave, linalopakana na Jangwa la Bonde Kuu, ikihisiwa kuwa mahali hapo ni penye joto zaidi Duniani wakati wa kiangazi.
Bonde la Death Valley ndilo eneo la mwinuko wa chini kabisa katika Amerika Kaskazini, katika futi 282 (86 m) chini ya usawa wa bahari.
Hiyo ni maili 84.6 (136.2 km) mashariki-kusini-mashariki mwa Mlima Whitney ambayo ni sehemu ya juu zaidi Marekani yenye mwinuko wa futi 14,505 (m 4,421).
Julai 10, 1913, Mamlaka ya Hali ya Hewa ya Marekani ilirekodi halijoto ya juu ya 134 °F (56.7 °C) katika bonde hilo la kifo, ambayo ni halijoto ya juu zaidi ya hewa iliyoko kuwahi kurekodiwa ya Dunia.
Hata hivyo, jambo hilo na mambo mengine kadhaa yaliyochukuliwa katika kipindi hicho kama rekodi yanapingwa na baadhi ya wataalamu wa kisasa wa Sayansi.
Kwenye Bonde hilo la Kifo la California, pia kuna mawe makubwa ambayo husogea kwenye ardhi ya jangwa, yakiacha njia ndefu nyuma yao pasipo hali ya kawaida.
Halafu kundi la mapainia wa Uropa na Amerika waliwahi kupotea katika majira ya baridi kali ya 1849-1850, walipokuwa ikitafuta njia ya mkato ya kuelekea kwenye mashamba ya dhahabu ya California.
Ingawa ni mmoja tu wa wanakikundi alikufa hapa, lakini wote walidhani kwamba bonde hilo lingekuwa kaburi lao.
Bonde la kifo ni makazi ya kabila la Timbiza la Wenyeji wa Marekani, ambao zamani walijulikana kama Panamint Shoshone, ambao wameishi katika bonde hilo kwa angalau milenia iliyopita.
Hata hivyo, licha ya tafiti nyingi, hakuna mtu aliyeng’amua moja kwa moja jinsi mawe hayo yanavyosogea na hadi sasa imebaki kuwa kitendawili.