Mafuriko makubwa yaliyotokana na Mvua zinazoendelea kunyesha, yameharibu miundombinu likiwemo Gereza la Mji wa Maiduguri Nchini Nigeria na kusababisha Wafungwa 270 kutoroka.
Wakisimulia hali ilivyo, Maafisa wa Magereza hilo wamesema, hata hivyo tayari Wafungwa saba wamerejea, huku kwa mara ya kwanza Serikali ikikiri kutoroka kwa wafungwa hao baada ya mafuriko hayo kuangusha kuta za jela.
Mafuriko hayo makubwa, pia yamesababisha maafa kwa watu 30 katika mji huo unaopatikana jimbo la Borno na kuwaacha maelfu bila makazi baada ya nyumba zao kusombwa kuzinguwa na kuharibiwa na maji.
Inaarifiwa kuwa, kuvunjika kwa kingo za bwawa la Alau, kulisababisha Wanyama wakali kama Mamba na Nyoka kusombwa na maji hadi kwenye makazi ya watu, baada ya Mvua kuharibu Mbunga ya Wanyama inayomilikiwa na Serikali.