Zimbabwe inapanga kuwaua Tembo 200, ili kulisha jamii zinazokabiliwa na njaa kali baada ya ukame mbaya kuwahi kutokea katika miongo minne, mamlaka ya wanyamapori,  itakayogawiwa kwa jamii zilizoathiriwa na ukame.

Msemaji wa Mamlaka ya Hifadhi na Wanyamapori Zimbabwe – ZIMPARKS, Tinashe Farawo alisema ugawaji huo utafanyika katika Wilaya za Hwange, Mbire, Tsholotsho na Chiredzi, hatua ambayo inaakisi uamuzi wa nchi jirani ya Namibia wa kuwaua ndovu 83 na kusambaza nyama kwa watu walioathiriwa na ukame mwezi Agosti 2024.

Ukame mkubwa uliojitokeza kutokana na mabadiliko ya Tabia nchi umesababisha migogoro kati ya binadamu na wanyamapori kuongezeka, ikikumbukwa mwaka 2023 mashambulizi ya tembo yaliwauwa watu 53.

Hata hivyo, ugawawaji wa Nyama hiyo unalenga kupunguza msongamano wa tembo katika mbuga za Taifa hilo, ambazo zina uwezo wa kuhimili Tembo 55,000 pekee tofauti na sasa ambapo zaidi ya Tembo 84,000 nchini Zimbabwe.

Rais Samia: Falsafa ya 4R imeliunganisha Taifa
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Septemba 18, 2024