Unaitwa Amazon, ni msitu wenye mambo mengi na historia kubwa Duniani ukiwa na kila aina ya vituko, wanyama wakali na vitisho, unaambiwa msitu huu ni hatari lakini kuna watu wanaishi humo

Sasa achana na yote uliyowahi kuyasikia kuhusu Msitu huu, ipo hivi – ndani kabisa ya msitu wa Amazon, kuna mlima uitwao Cerro El Cono.

Mlima huu ni wa kipekee na wa ajabu ukiwa katika eneo linalojulikana kama Sierra del Divisor au “The Watershed Mountains.”

Eneo hili ni maarufu kwa kuwa na Wanyamapori wa aina tofauti na ni nyumbani kwa baadhi ya makabila ya Asilia ambayo yanaishi humu kwa amani bila hofu.

Wenyeji huona mlima huu, wenye umbo la piramidi, kama jambo lao kubwa la kitamaduni na kiroho.

Wanana jina lao wanaita ‘Apu ya Andean’, ambayo hutafsiri kama roho inayowakilisha mlima na kuwalinda watu wanaoishi huko.

Tamaduni hii inarudi nyuma hadi wakati wa Milki ya Inca huko Peru, Ecuador, na Bolivia ambao nao waliabudu miungu ya namna hii.

Unaweza kuupata mlima huu wa baridi karibu na Pucallpa mashariki mwa Peru, karibu na Mto Ucayali, ambao ni tawi muhimu la Mto Amazon, “VISIT AMAZON” usijali lakini ukiweza umeweza.

Maisha: Hii hapa Dawa ya migogoro ndani ya ndoa
Mlipuko vifaa vya mawasiliano wauwa 9, maelfu wajeruhiwa