Mkurugenzi wa kampuni ya Mati Super Brands limited iliyopo mkoani Manyara na mdhamini mkuu wa timu ya Fountain gate, David Mulokozi amezindua tawi la Fountain gate royal fans mjini Babati ikiwa ni ishara ya kuikaribisha timu hiyo mkoani Manyara.

Akizungumza katika hafla hiyo Mulokozi amesema ujio wa timu hiyo ni fursa kubwa ya kiuchumi kwa wanamanyara hasa kwa wafanyabishara wakubwa pamoja na wadogo lakini yeye kama mdhamini mkuu ananufaika Sana kwani fursa ya kibiashara.

Aidha amewasihi mashabiki na wapenzi wa mpira wa miguu mkoani Manyara kujitokeza kwenye Kila mchezo wa ligi kuu utakaochezwa kwenye uwanja wa Tanzanite Kwaraa dhidi ya timu ya Fountain gate Fc na kulingana na idadi kubwa ya watu waliojitokeza kwenye michezo ya awali ameuomba uongozi wa mkoa kuongeza majukwaa, ili kuingiza idadi kubwa zaidi ya Watazamaji.

” Tunakiwa tujaze uwanja siku timu yetu itakapocheza na tunamuomba mkuu wa mkoa atuongezee majukwaa kwa kuwa hayatoshi, kwasababu mwamko wa watu kujitokeza uwanjani ni mkubwa sana.”

Kwa upande wa mashabiki wa Fountain gate waliojitokeza kwenye uzinduzi wa tawi wa tawi wamesema wamefurahishwa na tukio Hilo na kuomba yasiishie kwenye maneno badala yake wajikite kwenye vitendo zaidi ili tawi lisonge mbele.

Uzinduzi wa tawi la Fountain gate royal fans ni wa kwanza kufanyika tangu timu hiyo ipande ligi kuu na kuchagua uwanja nyumbani kuwa wa Tanzanite Kwaraa na kwasasa inaongozwa kauli mbiu isemayo “Timu moja, Timu pamoja

Kigoma mbioni kufaidi fursa za kiuchumi
Watakaokiuka taratibu za uchaguzi kukiona