Wanamwita “Coffin Confessor” lakini jina lake halisi ni Bill Edgar raia wa Australia, alipewa jina hilo la utani kutokana na kazi yake ya kutangaza siri za marehemu wakati wa mazishi.
Ni mfanyabiashara aliyefanikiwa, mshauri, mwandishi na mmoja wa wapelelezi wakuu wa kibinafsi wa Australia, ambaye anajulikana kwa kufanya kile ambacho wanasheria, wahasibu na wataalamu wengi hawawezi kufanya au wanaogopa kufanya.
Bill anasema Watu ambao wanakaribia kufa humuita na kumwambia siri nzito ambazo hawawezi kuzisema wao wenyewe na kulipwa kiasi cha dola 10,000.
Kuna wakati aliwahi kufanya mahojiano, akijibu maswali ya Mwandishi alisema ana siri nyingi za wateja ambao anasubiri wakifa akazitangaze kwenye misiba yao.
Anadai moja ya siri nzito aliyonayo ambayo inampa tabu na anadhani italeta taharuki, ni ile ya Mwanaume mmoja aliyekuwa na mahusiano na mke wa kaka yake.
Story nzima ipo hivi, watu hufikiria upo muda watakufa na hawataki kufa na siri na hawajawahi kuwa na ujasiri wa kuwaambia marafiki au familia zao.
Sasa kuna mtu anayeweza kutunza yote hayo, ambaye hana heshima kwa walio hai, ambaye atafanya lolote kwa ajili ya wafu ambaye kaamua kujilipua kwa kuzichukua na kusubiri wakifa aweze kuzitoa hadharani.
Ndiye Bill Edgar, mkali wa hizo mambo na mtaalamu wa kipekee aliye na dhamira ya kujibu maombi haya ya mwisho kwa niaba ya wateja wake ambao wataaga dunia hivi karibuni.
Bill amekuwa na mambo mengi katika maisha haya wasifu wake ukiwa ni mwana wa mmoja wa majambazi mashuhuri wa Australia, mtoto wa mitaani asiye na makao, mfungwa mwenye ulinzi mkali, mtu mgumu.
Ni mwanafamilia mwizi wa magari, fundi wa kupiga ngumi kitaaluma, mwanafalsafa, mvumbuzi, mpelelezi binafsi, mwathirika wa unyanyasaji wa kijinsia wa kutisha wa utotoni na mwanaharakati anayepigania kuangusha taasisi zinazoruhusu hali hiyo na Mwokoaji
Kukabiliana na mambo ya kutatanisha, kufurahisha na kuhuzunisha moyo ni moja kazi zake, maisha aliyoishi kando ya jamii, pande zote za sheria na kile ambacho kinaweza kukufundisha kuhusu yeye basi yupo tayari.
Sema kuna wana wanajiuliza yeye siri zake yupo tayari kumpatia mtu ili azimwage hadharani siku atakapoona yupo tayari kuziachia kabla hajafa? Muda utaongea.