Johansen Buberwa – Kagera.

Wakala wa Nishati Vijijini REA, imemkabidhi Mkandarasi wa kampuni ya CCC International Engineering Nigeria Limited mradi wa kufunga huduma ya umeme kwenye vitongoji 135 Mkoani Kagera ndani ya miezi 24, wenye thamani ya shilingi bilioni 14.8

Akizungumza wakati wa kukabidhi mradi huo Mhandisi wa REA Kanda ya ziwa, Ernest Makale amesema kupitia muradi huo kila jimbo litanufaika kwa vitongoji 15 kufungiwa huduma ya umeme na kila kitongoji kitajengwa transformer ya ukubwa KVA 100.

Mkuu wa wa Mkoa wa Kagera, Hajjat Fatma Mwassa amewaasa wanchi kutoa wa mkoa huo kutoa ushirikino wa kutosha kwa mkandarasi huyo anayetekeleza mradi huo huku akimtaka mkandarasi atekeleze muradi huo kwa weredi na kukamilisha kwa muda uliopangwa maana hapo awali imekuwa changamoto kwa baadhi ya wakandarasi wengine kushindwa kukuamilisha miradi ya serikali kwa wakati.

Amesema, “tulikuwa na vitongoji 3600 kati ya hivyo 1500 kazi yake ilikamika na vingine 2000 hajafikiwa na huduma ya umeme hivyo tunaomba kama Mkoa wa Kagera mtendaji mkuu wa Rea atusadie kuleta kambi ya watumishi wakutosha ili kusimamia mradi huu ukamilike kabla ya uchaguzi mkuu.”

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa kata ya Katerero kijiji Bulaya waliozungumza na Dar24 media akiwemo Siliver Katabaro na Rosemary Patrick wameishukuru Serikali kwa kawaletea mradi huo kwani itawasaidia kuleta fursa mbalimbali huku wakiiomba serikali kupunguza bei ya kununua nguzo za umeme kipindi wanapohitaji kuweka huduma hiyo majumbani mwao.

Serikali yatimiza ahadi ugawaji Mahindi Msomera
Mchengerwa atoa maagizo ujenzi Longido Samia Girls