Klabu ya Simba imeendelea kuandika Historia katika soka la Afrika baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Al Ahly Tripoli mchezo wa raundi ya pili kufuzu hatua ya makundi kombe la Shirikisho. Ushindi huo umeifanya Simba ifuzu moja kwa moja hatua za makundi ya Shirikisho ikiwa ni mara ya 6 kwa klabu hiyo kufuzu hatua hiyo tangu msimu wa 2017/18.
Katika mchezo huo mgumu uliopigwa Dimba la Benjamini ni Mabululu kutoka Ali Ahli alikuwa wa kwanza kufunga bao la uongozi dakika ya 16 ya mchezo , Bao hilo lilidumu mpaka dakika ya 36 ambapo Kibu Denis alisawazisha na dakika ya 45+1 Ateba aliwapa Simba bao la pili. Mpira ulikwenda mapumziko Simba wakiongoza kwa mabao 2-1.
Kipindi cha Pili kilikuwa tofauti na kipindi cha kwanza baada ya mwalimu Fadlu kuwapumzisha baadhi ya nyota kama Kibu Denis na Yusuf Kagoma kisha kuwapa nafasi Awesu Awesu na Edwin Balua aliyewapa furaha mashabiki wa Simba kwa kufunga bao la tatu dakika ya 90+2 na Simba kuondoka na ushindi wa mabao 3-1.
Kibu Denis,Joshua Mutale ,Debora Fernandez,Moussa Camara na Ateba ni majina yaliyopasua mioyo ya mashabiki na wachezaji wa Al Ahli kutokana na usstadi wa kuumiliki mchezo na kutengeneza nafasi ndani ya uwanja. Nyota hao wamekuwa na mwendelezo mzuri kwa mechi nne walizocheza mpaka sasa .