Maisha ni mojawapo kati ya masuala makuu kuhusu thamani, madhumuni na umuhimu wa binadamu kuwepo duniani na vile ambavyo amejaaliwa kuishi.

Maana ya maisha imechanganyika kwa undani na dhana za falsafa na imani za dini na hugusia masuala mengine mengi, kama vile ontolojia, tunu, kusudi, maadili, hiari, uwepo wa Mungu, roho, na kinachoendelea baada ya kifo.

Zifuatazo ni mbinu mbalimbali ambazo zinaweza kukusaidia kufurahia maisha yako ya kila siku kiasi ukatengeneza nuru na kuhuisha mafanikio yako.

1. Kumbuka kila wakati kuwa hakuna mtu kwenye hii ardhi ya Dunia ambaye hana shida ma wewe si pekee ambaye una matatizo.

2. Changamoto ni sehemu ya maisha na mtu pekee ambaye hana changamoto ni yule aliyekufa.

3. Hakuna tatizo ambalo halina ufumbuzi, kuna suluhisho kwa maumivu unayopitia hivyo usikate tamaa.

4. Jinsi unavyopiga picha akilini mwako, au kile unachofikiri, kinaweza kuathiri furaha yako. Jifikirie kama mtu wa thamani na epuka ubinafsi.

5. Usijali kuhusu watu wanasema nini juu yako. Baadhi ya watu ni wanaweza kusema tu mambo ya kukufanya uhisi huzuni, wapuuze.

6. Fanya urafiki na watu wenye akili timamu wanaofanya uwe furaha. Usifanye urafiki na watu ambao
kukufanyia mzaha au kukucheka juu ya changamoto zako.

7. Wakati wako utumie kwa shughuli nyingi za mambo unayopenda zaidi kama vile michezo, kutazama sinema, kuvinjari mtandaoni, kucheza kompyuta nk.

8. Usiruhusu mtu yeyote akuogopeshe na pesa au vitu vya kimwili. Mtu maskini leo anaweza kuwa tajiri kesho. Mabadiliko ni mara kwa mara.

9. Haijalishi unapitia nini leo, usikate tamaa. Palipo na maisha, kuna matumaini.

10. Omba sana. Omba bila kukoma. Maombi ni kichocheo kinachoweza kukuharakisha baraka zije kwako kwa wakati. Kuwa jasiri nenda na kile unachotaka kiwe.

Muliro: Waliokamatwa walikaidi katazo la Polisi
Lugha 57 za 'Things Fall Apart' ya Chinua Achebe