Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamisha Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Muliro Jumanne amesema watu wema wanaitamani mitutu ya Bunduki na kwamba hitaji lao ni kuona ipo mpaka maeneo wanayoishi kwakuwa hawana uhusiano nayo kiuhalifu, bali inawalinda.

Muliro ameyasema hayo hii leo Septemba 23, 2024 wakati akizungumza na Vyombo vya Habari na kuongeza kuwa wanaoshangaa kuona magari na Polisi wenye mitutu ni wale wenye vimelea vya uhalifu, huku akisisitiza juu ya doria wanazozifanya kuwa zinatakiwa ziendelee kudumu.

Amesema, “Mtu mwema anafurahi sana kuiona hiyo unayoiita mitutu, kwasababu haina uhusiano na yeye. Wanatamani iwe mpaka mlangoni, watu wema wanataka amani wanataka usalama. Watu wanaoshangaa ni watu wenye vimelea vya uhalifu lakini watu wazuri wanatamani hali hii iende mpaka kule waliko chini.”

Muliro aliyasema hayo wakati akijibu swali la Mwandishi na kutoa taarifa juu ya kukamatwa kwa watu 14, wakiwemo Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA, Mwenyekiti Freeman Mbowe, Makamu Mwenyekiti, Tundu Lissu, Godbless Lema na Peter Lazaro ambao amesema wanaendelea kuhojiwa kwa kuzingatia misingi ya kisheria.

Rais Samia katika ufunguzi Tamasha la Utamaduni la Kitaifa
Wananchi msiwe na hofu, endeleeni na shughuli - Polisi