Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Mahundi amewataka maafisa Uhusiano kuendelea kufanya kazi kwa manufaa ya maendeleo ya Nchi na Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Ujumla.

Mhandisi Mahundi ameyasema hayo jijini Arusha wakati akifungua Mkutano Mkuu watatu wa Umoja wa Maafisa Uhusiano katika Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika katika Ukumbi wa Lush Garden.

Akiwa katika Mkutano huo Mhandisi Mahundi amezindua Ofisi za Umoja wa Maafisa Uhusiano katika Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo Makao Makuu yake yatakuwa jijini Arusha.

Akina Nyundo wakutwa na kesi ya kujibu
SMZ kuleta mageuzi sekta ya Elimu