Hotuba za Viongozi mbalimbali wa dunia, ambazo wamezitoa katika mkutano wa Hadhara Kuu ya Umoja wa Mataifa zimeutahadharisha ulimwengu juu ya kuanza kutanuka kwa vita vya Mashariki ya Kati.

Takribani viongozi wote wakiwemo wa Mataifa makuu, wamekuwa wakizungumza tangu kufunguliwa kwa mkutano huo wa 79 Septemba 24, 2024 wakijielekeza kwenye mzozo huo wa Mashariki ya Kati kutokana na kukithiri kwa mashambulizi.

Aidha, wengi wao wamekosoa mashambulizi ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza na Lebanon, wakisema haki ya kujilinda imegeuka kuwa kisasi na inazuia kufikiwa kwa makubaliano ya kuachiliwa kwa mateka na kusitisha mapigano.

Baadhi ya Viongozi hao, ni pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Gutteres, Rais wa Marekani, Joe Biden, Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, Kiongozi wa Qatar, Sheikh Tamin bin Hamad Al-Thani, Rais wa Baraza la Ulaya, Charles Michel na Rais Masoud Pezeshkian wa Iran.

Awali, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, alisema hali ya uhalifu, kutokuchukuliwa kwa hatua, ukosefu wa usawa na wa uhakika unaufanya ulimwengu wa sasa kukwama kushughulikia janga hilo.

Kwa upande wake, Balozi wa Israel kwenye Umoja wa Mataifa aliuita mkutano huo kuwa ni kituko cha mwaka cha unafiki, huku akisisitiza kuwa nchi yake haina haja ya kutuma wanajeshi wa ardhini kwenye nchi ya kigeni.

Wosia wa Charlie Champlin kwa Walimwengu
Kapinga: Ushirikiano Sekta ya Maji umeleta mafanikio