Shirika la haki za Binadamu la Amnesty International, linatarajiwa kuwasilisha ombi la kuundwa kwa tume itakayochunguza vifo vya watu kadhaa vilivyotokana na Polisi kutumia nguvu kupita kiasi kinyume cha sheria, wakati wa maandamano yaliyofanyika miezi mitatu iliyopita Nchini Kenya.
Hatua hiyo, inakuja baada ya Wazazi wa waandamanaji kukusanyika nje ya Wizara ya Sheria mapema siku ya Jumanne Septemba 24, 2024 kuwasilisha orodha ya waliouawa katika maandamano yaliyofanyika kati ya Juni na Agosti, 2024.
Hata hivyo, wanaharakati na Mashirika ya haki za binadamu yanadai kuwa zaidi ya Watu 60 waliuawa wakati maandamano, yaliyokuwa yakipinga muswada wa fedha uliopendekeza nyongeza ya ushuru na matukio ya kutoweka kwa Watu wiki kadhaa baada ya maandamano.
Maandamano hayo ya liyoongozwa na Vijana maarufu kama Gen Z, yanadaiwa kuwa yalileta upinzani mkubwa dhidi ya rais wa Taifa hilo, William Ruto na wengi walidai kuna ufisadi na matumizi mabaya ya fedha za umma.