Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewahakikishia Wawekezaji kutoka Korea ya Kusini kuwa Zanzibar ina fursa nyingi za Uwekezaji na kuwakaribisha.
Dkt. Mwinyi aliyasema hayo Ikulu alipokutana na Mkurugenzi Mkaazi wa Taasisi ya Korea Overseas infastructure and Urban Development ya Korea Kusini (KiND), Kim Jong Hoon.
Ameuambia Ujumbe huo kuwa Serikali Imefungua milango ya Uwekezaji na Ushrikiano kwa Taasisi zenye nia za kuwekeza nchini na Kuwasisitiza Wawekezaji kutoka Korea kuwekeza Zanzibar.
Rais Mwinyi ameelezea kufarijika kwa taasisi hiyo kuwa na Wazo la kuwekeza hapa nchini hususan katika Mradi wa Mchezo wa Maji, kuwa Wazo zuri na lenye tija huku akiuhakikishia Ujumbe huo kuwa Serikali itatoa Ushirikiano wa kutosha kwa taasisi hiyo ili lengo la Mradi lifanikiwe.
Naye Kim Hoon alieambata na Bibi Yoko Eunna ambaye ni Makamu wa Rais wa Kampuni ya Usarifu ya Heerim ya Korea amesema Taasisi hiyo ina uzoefu mkubwa wa uwekezaji katika miradi tofauti katika nchi za Afrika ikiwemo Ethiopia na Kenya kwa sasa imevuka kuwekeza Tanzania ikiwemo Zanzibar.

Kapinga: Ushirikiano Sekta ya Maji umeleta mafanikio
Katimba: DART timizeni majukumu, fanyeni kazi kwa bidii