Ganga Zumba (1630 – 1678), mwamba wa himaya inayojulikana na wengi kama African Spartacus, Kiongozi wa kwanza wa makazi makubwa ya watumwa waliotoroka ya Quilombo dos Palmares, au Angola Janga, katika jimbo la sasa la Alagoas, Brazili.

Zumba mzaliwa wa Kongo, alikamatwa na kufanywa mtumwa na baadaye kutoroka utumwani kwenye shamba la miwa na hatimaye akapanda hadi cheo cha juu kabisa ndani ya ufalme wa Palmares huko Brazil wakati akifanya kazi kama mtumwa wa shamba la Miwa.

Baadaye alifanikiwa kutoroka, kisha akaliinua jeshi la Waafrika waliokuwa watumwa na kuanzisha ufalme wake wa Palmares, Ikulu na Mahakama.

Ganga Zumba anakumbukwa na wanahistoria kama shujaa Mweusi na mpigania uhuru ambaye alikuwa kiini cha historia na mapambano ya kisasa ya Vuguvugu la Watu weusi huko Brazil baada ya kuongoza muungano wa “makazi huru” huko Quilombo dos Palmares.

Himaya yake inapatikana katika majimbo ya Alagoas na Pernambuco, kaskazini-mashariki mwa Brazili, Quilombo dos Palmares ilianzishwa na Waafrika wa mapema wa Brazili mwishoni mwa karne ya 16 kama upinzani dhidi ya wakoloni wa Ulaya na watumwa.

Ni moja ya maeneo ya kwanza, katika Amerika, ambapo watu weusi waliletwa kwenye Ulimwengu Mpya wakiwa watumwa, na baadaye walipata uhuru ambapo kwa karibu miaka 100, Watu Weusi huko Quilombo walipigana dhidi ya watumwa wao, hasa Wareno ambao walijaribu kuitawala Brazili.

Zumba, kama mfalme wa Quilombo katika miaka ya 1670, aliongoza mashambulizi haya dhidi ya watumwa na licha ya vitisho vya mara kwa mara kutoka kwa mamlaka ya kikoloni, Quilombo alikuwa imara na kama watumwa watoro walianzisha uchumi wa pamoja unaotegemea kilimo cha kujikimu, biashara na umiliki wa ardhi ya jumuiya.

Kufikia miaka ya 1670, Ganga Zumba alikuwa na Kasri, wake watatu, Walinzi, Mawaziri, na watu waliojitolea katika boma lake la kifalme lililoitwa Macaco. Macaco linatokana na jina la mnyama (Tumbili) ambaye aliuawa na wakati wa uhai wake alipendwa sana na raia.

Kiwanja chake chenye kasri kilikuwa na nyumba 1,500 ambazo ziliishi familia yake, walinzi, na maafisa, ambazo zote zilizingatiwa kuwa za kifalme. Alipewa heshima ya Mfalme na heshima ya kutosha.

Mwaka 1678 Zumba ilikubali mkataba wa amani uliotolewa na Gavana Mreno wa Pernambuco, ambao ulihitaji kwamba wana Palmarino wahamie kwenye Bonde la Cucaú. Katika mkataba huo, Wareno walithibitisha kukubali kwao Zumba kuwa Kiongozi mkuu wa watu wake.

Baadaye 1679, mkataba huo ulipingwa na Zumbi na mmoja wa wapwa wa Ganga Zumba, ambaye aliongoza uasi dhidi yake akiakisi uasi wa Zumbi dhidi ya majaribio ya Wareno ya kugawa upya ardhi ya Palmares kwa miongoni mwa maafisa wa Ureno.

Katika mkanganyiko uliofuata, migogoro na usaliti, ilipelekea Ganga Zumba kulishwa sumu na mmoja wa jamaa zake mwenyewe kutokana na kitendo chake cha kuingia mkataba na Wareno na ilifahamika baadaye kuwa Joao “mulatto”, Gaspar na Amaro walihusika kumuua Zumba.

Hapo sasa kilichofuata ni Wafuasi wake wengi ambao walikuwa wamehamia kwenye Bonde la Cucaú, kurudishwa tena utumwani na Wareno.

Kwa heshima yake, Filamu ya Kibrazili ya Ganga Zumba ilitengenezwa mwaka wa 1963 lakini haikutolewa hadi 1972 kwa sababu kulikuwa na mapinduzi ya kijeshi nchini Brazili mwaka wa 1964 na filamu kuhusu mapinduzi, hata yale yaliyotokea katika karne ya 17, zilizingatiwa kuwa hatari kisiasa.

Filamu hiyo inatokana na riwaya ya João Felício dos Santo, ikiangazia mtumwa mweusi ambaye anaishia Palmares na ilihusu ukombozi wa watu weusi ikiweka mtazamo wa rangi nyeusi.

Wazee wahimizwa kufanya mazoezi kuimarisha Afya
Kijiji wanachoishi Wachawi 96 pekee, wana tuzo za mwaka