Kamati mbili za Kudumu za Bunge za ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu zinawaalika Wadau kutoa Maoni kuhusu Miswada miwili ya Sheria.
Taarifa ya Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa imeeleza kuwa maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria ni yale ya Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.3) wa Mwaka 2024 [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No. 3) Bill. 2024].
Kwa upande wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu yenyewe itapokea maoni ya Muswada wa Sheria ya Shirika la Utangazaji Tanzania wa Mwaka 2024 ambapo Kamati zote mbili zitapokea na kusikiliza Maoni ya Wadau (Public Hearing) Oktoba 17, 2024 kuanzia Saa 4:00 Asubuhi.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria yenyewe itapokea Maoni kwenye Ukumbi wa Frank Mfundo, Ghorofa ya Tano, Jengo la Utawala Ofisi ya Bunge, Dodoma huku Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ikipokea Maoni katika Ukumbi Na. 231, Ghorofa ya pili Jengo la Utawala, Ofisi ya Bunge, Dodoma.
Kamati hizo zinawaalika wadau wote wenye maoni kuhusu Miswada hiyo kufika na kuwasilisha Maoni yao kabla Miswada hiyo haijapelekwa katika hatua nyingine ambapo maoni hayo pia yanaweza pia kuwasilishwa kwa njia ya Posta kupitia anuani ya Ofisi ya Bunge au kupitia Barua pepe na Miswada husika inapatikana katika tovuti ya Bunge ya www.bunge.go.tz.