Afarah Suleiman, Babati – Manyara.
Wananchi Wilayani Babati Mkoani Manyara ambao wamekidhi vigezo vya kupiga kura, wamehimizwa kujitokeza kwa wingi na kushiriki kikamilifu kwenye zoezi la uandikishwaji wa wapiga kura ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Novemba 2024.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Msimamizi wa Uchaguzi ambae pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati CPA Shaaban Mpendu amesema Kwa mujibu wa Sheria wakazi wote waliozimiza umri wa miaka 18 na Zaidi wanahimizwa kushiriki kwenye Uchaguzi huo kwa kuchukua fomu za kugombea au kupiga kura.
Amesema, “ninatoa wito kwa wananchi wote kushiriki kikamilifu katika mchakato huu wa Uchaguzi kuanzia katika hatua ya kujiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura,ni hatua muhimu inampa Kila mwananchi sifa na haki ya kisheria kushiriki Uchaguzi kama mpiga kura au mgombea.”
Kwa upande wake Katibu Tawala Wilaya ya Babati, Halfan Matipula amewataka wananchi kushiriki uchaguzi huo Kwa amani na utulivu huku akiwataka viongozi wa vya siasa kuelemisha wanachama wao kufanya uchaguzi wa haki.
“Nawaombeni pitieni ratiba ya Uchaguzi,kafanyeni hivyo waelimisheni na wanachama wenu ili Uchaguzi wetu uwe wa haki na salama, Uchaguzi ni gharama fedha zinazotumika ni fedha za wananchi za watanzania asitokee mtu kuvuruga Uchaguzi kwa sababu zake binafsi,” amesema.
Kwa upande wake Mkuu wa Polisi Wilaya ya Babati, Ernesta Mwambinga amesema kila Mwananchi anapaswa kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi endapo akiona kuna viashiria vya uvunjivu wa amani na kuwataka kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha usalama unakuepo Kila wakati.
Amesema, “Kila tutakapoona kuna kiashiria Cha vurugu sio tusubirie adi zitokee basi thakikishe tunadhibiti wote kwa pamoja lakini pia tuhakikishe tunakua na amani mda wote niwaombe pia wagombea na Viongozi wa vyama vya saisa wafate Sheria na taratibu za Uchaguzi.”