Taarifa kutoka Wizara ya Afya ya Lebanon imesema karibu watu 700 ndani ya wiki hii wameuawa kutokana na Mashambulizi ya Israel na kufanya jumla ya watu waliopoteza maisha kufikia 1,540 katika kipindi chote cha mapigano, huku Ujerumani ikitangaza kuunga mkono juhudi ya kusitishwa mapigano nchini humo.

Hatua hiyo imepelekea Maafisa waandamizi wa Israel kutishia kurudia mashambulizi kama ilivyotokea kwa Gaza katika ardhi ya Lebanon, ikiwa Hezbollah wataendelea na mashambulizi yao.

Hata hivyo, Shirika la Kimataifa la Uhamiaji lilikadiria kuwa zaidi ya watu 200,000 wameyakimbia makazi yao nchini Lebanon tangu Hezbollah kuanza kufyatua roketi kuelekea upande wa kaskazini wa Israel, kwa lengo la kuunga mkono Hamas baada ya kuvamiwa na vikosi vya Israel.

Hata huvyo, Mataifa mbalimbali bado yanaendelea kutoa wito wa kusitishwa mapigano kwa siku 21 huku Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Annalena Baerbock akisema Israel na Wanamgambo wa Hezbollah wa Lebanon wanapaswa kukubaliana na pendekezo hilo mara moja.

Babati: Waliokidhi vigezo wahimizwa kujiandikisha