Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,  Mhandisi Maryprisca Mahundi ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya na Mkurugenzi wa Maryprisca Women Empowerment Foundation (MWEF) ametekeleza ahadi yake ya kuwasaidia wafungwa na mahabusu Gereza la Ruanda lililopo Jijini Mbeya.

Mahundi amekabidhi vifaa vya michezo mipira na seti mbili za sare pamoja na tank la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita elfu tano Septemba 27, 2024.

Aidha Mahundi ameahidi kuendelea kuwaunga mkono kwa kuwanunulia magodoro pamoja na ujenzi wa bweni kwa ajili ya wafungwa wanawake.

Naye Mkuu wa Gereza hilo, Kamishina Msaidizi Sinjonjo Mwakyusa ameishukuru Taasisi ya Maryprisca Women Empowerment Foundation pamoja na Ofisi ya Mbunge Mhe. Mahundi kwa msaada alioutoa nakueleza kuwa utasaidia kuimarisha afya za wafungwa na mahabusu.

Wasichana 4,843 waripoti Shule maalum za Sayansi Mikoa
Matumizi Nishati safi ya kupikia: Afrika ibadilike - Rais Samia