Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewahimiza Waumini wa Dini ya kiislamu kutumia maadhimisho ya Kuzaliwa Mtume Muhamad (SAW) kuwafundisha maadili mema vijana na watoto.
Alhaji Dkt. Mwinyi ameyasema hayo katika Masjid Ayytul Kisauni Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini Magharibi alipojumuika katika sala ya Ijumaa.
Amesema vitendo Viovu vinavyotokea katika jamii hivi sasa vinachangiwa kwa kiasi kikubwa kwa vijana kukosa maadili na tabia njema.
Alhaji Dkt. Mwinyi amefahamisha kuwa ni vyema majukwaa ya Maulid yakatumika kuwafundisha vijana na watoto kutekeleza maadili mema ya kiislamu ili kuwa na jamii Bora.
Aidha amewasisitiza Waumini wa dini ya kiislamu kudumisha Amani na Utulivu ili Serikali itekeleze mipango ya Maendeleo.