Shirika la Kukuza Biashara Duniani (WTPO), limetangaza kutoa tuzo mwaka huu 2024, ambapo Mamlaka Maendeleo ya Biashara nchini Tanzania TANTRADE imeorodheshwa kuwania tuzo hiyo ya kuwa Shirika bora linalokuza biashara katika kipengele cha Matumizi bora ya Teknolojia ya Habari.
TANTRADE ni miongoni mwa mashirika nane ya kitaifa ya kukuza biashara yaliyoteuliwa na kituo cha biashara cha kimataifa cha (ITC).
Kupitia taarifa iliyotolewa 30 Septemba 2024 na Kaimu mkurugenzi mkuu wa Tantrade Yusuph Tugutu imeeleza kuwa lengo la tuzo hizo ni kuangazia na kuainisha mipango ya muda mrefu na wa kati.
Mipango hiyo ni ya maendeleo ya biashara na mauzo nje ya nchi Iikiwa ni pamoja na kuboresha utendaji kazi wa mashirika ya kutangaza biashara TPO na kuzipa nguvu na uwezo wa kiushindni biashara zinazouza soko la nje.
Aidha, Mkurugenzi mkuu wa TANTRADE Latifa Mohamed Khamis amesema kwamba wameweka mkakati wa uwazi wa mazingira ya kibiashara yatakayohamasisha kukuza ushirikiano wa kibiashara kimataifa.
TANTRADE pia imeteuliwa kuwania kipengele cha ‘ matumizi bora ya teknolojia ya habari miongoni mwa mashirika mengine matatu yatakayowania kipengele hicho.