Amina Omar, Tanga.

Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga, Mhandisi Juma Hamsini amesema uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024 utazingatia 4R za Rais Samia, huku akiwaita mezani wadau wa siasa, ili kuweka mikakati itakayofanikisha Uchaguzi huo kuwa huru na haki kwa vyama 19 shiriki.

Akizungumza na Waandishi kuhusu kuelekea kwenye uchaguzi huo, Mhandisi Hamsini alisema kwa Jiji la Tanga kuna mitaa 181 na kata 27, huku akiwahimiza Wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi huo,

Amesema, “tunawaomba Wananchi wajitokeze kushiriki Uchaguzi huu,kila mwananchi mwenye sifa anayo haki yakuchagua na kuchaguliwa, hivyo nawaomba Wananchi wajitokeze kwa wingi kushiriki Uchaguzi huu ili kutimiza haki yakikatiba.”

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Tanga, Mhandisi Juma Hamsini akizungumza na Waandishi wa Habari, kuhusu Uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.

Mhandisi Hamsini ameongeza kuwa, katika uchaguzi ni lazima uangalia tathimini za chaguzi zilizopita lakini wa mwaka huu utakuwa huru ,Haki na Amani .

“Lakini niwaambie kwamba Rais Dkt Samia Suluhu amehakikisha bajeti yetu tulioomba tumepatiwa kama ilivyokusudiwa hii inaonyesha uchaguzi huo ni huru na haki,“ alisema.

Hata hivyo, amesema ili uchaguzi uweze kuwa mzuri lazima kuwe na uwiano sawa kwa wadau wote wanaoshiriki uchaguzi kupitia vyama vyote kuanzia kwenye ngazi ya Mtaa,Kata mpaka Halmashauri washirikishwe kikamilifu nao wanafanya hivyo.

Aliwaeleza wananchi kuwa uchaguzi huo unasimamiwa na TAMISEMI, hivyo ni muhimu kila mkazi ajiandikishe kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na kwamba kwenye mtaa lazima kuwepo na nafasi za wajumbe, ili Mwenyekiti awe kamilifu kwa kuwa na wajumbe na Katibu wake ambaye ni Mtendaji wa Mtaa.

Waliotumwa na Afande waswekwa jela maisha