SOMO LA UVUMILIVU:

Kwanza tupate maana ya uvumilivu, hii ni hali ya kungojea kitu au jambo hadi litokee au litendeke, pasipo kujali urefu wa muda au mabadiliko ya kimazingira.

Uvumilivu unahusisha akili na moyo wetu, au namna tunavyotenda tunapokabili hali ngumu. Mtu anayevumilia anaonyesha sifa ya ujasiri, uimara, na subira.

Kuvumilia kunamaanisha pia uvumilivu licha ya magumu, kuteseka kwa subira bila kukata tamaa ukiwa unalenga kufikia aina ya jambo fulani kimafanikio bila kujari litachujua muda gani.

Bila shaka unalifahamu tunda la Pera, Mapera yote mawili ambayo unayaona katika picha hapo juu yakining’inia pamoja kwenye tawi la mti, moja tayari limeiva, wakati jingine linahitaji muda zaidi wakuiva.

Asili ya mapera haya inatufundisha somo muhimu sana maishani kwamba tunapoona wengine wanaotuzunguka wanapata mafanikio huku sisi hatujafanikiwa, haimaanishi kuwa hatutafanikiwa.

Hiyo inamaanisha kwamba wakati unaofaa kwetu bado haujafika, hivyo ni lazima tuwe na subira na tusikate tamaa kwa sababu ya kufadhaika.

Tunaweza kuwa na siku chache tu kabla ya kufikia hali yetu ya kukomaa na kumbuka kwamba, wakati wako utakuja, pia, lakini unahitaji uvumilivu na usubiri wakati sahihi.

REA kushiriki Samia Kilimo Biashara Expo 2024 Morogoro
Mazingira: Nishati safi ya kupikia italeta mageuzi - Mahundi