Zaidi ya shilingi bilioni 6.7 zimetumika katika ujenzi wa shule za Sekondari 10 zilijengwa katika kata 10 kati ya 13 za Wilaya ya Muheza mkoani Tanga katika kipindi cha maka mitatu ambazo zimesogeza huduma kwa wakazi wa maeneo hayo ambao watoto wao walikuwa wanatembea umbali mrefu kwaajili ya masomo sababu iliyokuwa inasababisha matokeo mabaya katika mitihani ya Elimu ya sekondari.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Zainab Katimba katika uzinduzi wa Kampeni ya Mtoto wa Leo Samia wa Kesho iliyolenga kuibua vipaji vya watoto na kuwatambua watoto wenye ulemavu katika wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga na mgeni rasmi akiwa ni . Naibu Waziri Mkuu na Waziri Nishati, Dkt. Doto Biteko.
“Hapo awali kulikuwa na kata 13 ambazo hazikuwa na shule za sekondari lakini alivyoingia madarakani Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshaleta fedha ambazo zimejenga shule za sekondari katika kata 10 na mwaka huu wa bajeti kuna kata
nyingine ya Kwezitu ambayo na yenyewe imeletewa milioni 580 kwaajili ya kujenga shule ya sekondari na tafsiri yake ni zimebaki kata mbili tu.”
Amesema, seikali inaendelea kuimarisha sekta ya elimu kwa kuendelea kutoa mafunzo kwa walimu na kuwajengea nyumba za kuishi ili wheeze kufanya kazi kwa bidii na ubunufu katika sekta ya elimu.
Akizungumzia mafanikio katika sekta ya Elimu katika Jimbo la Muheza,mbunge wa Jimbo hilo Hamis Mwinjuma amesema ndani ya miaka mitatu jumla ya vyumba vya madarasa 212 na amemshukru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa alama aliyoiweka katika wilaya ya Muheza.
Akihutubia wananchi wa Muheza waliojitokeza katika uzinduzi wa kampeni ya Mtoto wa Leo Samia wa Kesho Naibu Waziri Mkuu na Waziri na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amehimiza wananchi kuendelea kuilinda miundombinu hiyo huku akiwataka walimu kuwa wabunifu katika ufundishaji ili watoto wapate uelewa na kuwapata Samia wa kesho.

NLD yaitaka Serikali kuongeza muda wa Kampeni
Pumzika kwa amani DIKEMBE MUTOMBO, ulikuwa Binadamu