Boniface Gideon – Tanga.

Chama cha National League for Democracy (NLD), kimewasilisha ombi kwa serikali kuhusu kalenda ya uchaguzi iliyotolewa na Tamisemi,chama hicho kimeitaka Serikali kuketi na wadau wa Uchaguzi hususani vyama vya Siasa kuona namna wanavyoweza kuongeza muda wa kampeni.

Katibu Mkuu wa chama hicho, Doyo Hassan Doyo, awaeleza Waandishi wa Habari kuwa muda uliotolewa kwa maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji, na vitongoji ni mfupi sana nakwamba hautoshi,hivyo ni vyema Uchaguzi huo ukasogezwa mbele, huku akiitaka Serikali kukaa na wadau na kuona namna wanavyoweza kuongeza muda wa kampeni ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa haki na ufanisi bila vikwazo,

Amesema, “kupewa siku saba hadi siku kumi na nne, siku hizo haziwezi kutosha,wagombea wanahitaji muda mrefu wa kampeni Lakini pia Wananchi wanahitaji muda mrefu wa kuwachuja wagombea wao,hivyo Tunaiomba serikali kupitia Tamisemi isogeze mbele muda wa Uchaguzi, sio kuahirisha uchaguzi, bali kuongeza muda wa maandalizi.”

Wanachama zaidi ya 150 kutoka ADC na ACT wamejiunga na NLD na kupokelewa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Mhe. Doyo Hassan Doyo. Wanachama hao, wakiongozwa na Mariam Sijaona aliyekuwa mjumbe wa halmashauri kuu ACT Wazalendo na Scola Kahana aliyekuwa mgombea wa nafasi ya makamo mwenyekiti bara kupitia ADC na mgombea ubunge jimbo la kibaha katika uchaguzi wa 2020, wamejiunga na Chama cha NLD.

Doyo, pamoja na viongozi wengine wa NLD, akiwemo Makamo Mwenyekiti Bara, Mhe. Khamis Said Hamad, waliwakaribisha wanachama hao wapya na kuwahakikishia kuwa wana haki sawa na wanachama wa chama hicho kwa mujibu wa katiba ya NLD. Wanachama hao wamesema kuwa wameamua kujiunga na Chama cha NLD kwa sababu ni haki yao ya kikatiba na kuunga mkono juhudi za Mhe. Doyo katika kukuza demokrasia nchini.

Doyo Hassan Doyo, akizungumza na Waandishi wa Habari.

Doyo aliwasihi wanachama hao wapya kusoma Itikadi ya NLD, akisisitiza kuwa Itikadi ya chama hicho imebeba uzalendo, haki, na maendeleo.

Katika hatua nyingine Doyo alibainisha kuwa chama kinatarajia kufanya ziara ya kujitambulisha kwa wanachama pamoja na kutangaza sera za chama hicho nchini nzima ziara itakayoanza kuanzia Oktoba 30 ikianzia mkoani Tanga, Pemba, kanda ya ziwa na mikoa ya kanda ya kaskazini.

Wanachama zaidi ya 150 kutoka ADC na ACT wamejiunga na NLD na kupokelewa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Doyo Hassan Doyo. Wanachama hao, wakiongozwa na Mariam Sijaona aliyekuwa mjumbe wa halmashauri kuu ACT Wazalendo na Scola Kahana aliyekuwa mgombea wa nafasi ya makamo mwenyekiti bara kupitia ADC na mgombea ubunge jimbo la kibaha katika uchaguzi wa 2020, wamejiunga na Chama cha NLD.

Doyo, pamoja na viongozi wengine wa NLD, akiwemo Makamo Mwenyekiti Bara,Khamis Said Hamad, waliwakaribisha wanachama hao wapya na kuwahakikishia kuwa wana haki sawa na wanachama wa chama hicho kwa mujibu wa katiba ya NLD. Wanachama hao wamesema kuwa wameamua kujiunga na Chama cha NLD kwa sababu ni haki yao ya kikatiba na kuunga mkono juhudi za Doyo katika kukuza demokrasia nchini.

“Tunajua chama chetu kipya hakina ruzuku, lakini tupo tayari kukaa na njaa ili kupigania demokrasia ya kweli na hatimaye chama chetu kufanya vizuri kwenye chaguzi zijazo,” walisisitiza wana chama hao.

Doyo aliwasihi wanachama hao wapya kusoma Itikadi ya NLD, akisisitiza kuwa Itikadi ya chama hicho imebeba uzalendo, haki, na maendeleo.

Katika hatua nyingine Doyo alibainisha kuwa chama kinatarajia kufanya ziara ya kujitambulisha kwa wanachama pamoja na kutangaza sera za chama hicho nchini nzima ziara itakayoanza kuanzia Oktoba 30 ikianzia mkoani Tanga, Pemba, kanda ya ziwa na mikoa ya kanda ya kaskazini.

Wakati huo huo,Doyo amesema chama hicho kimepata Wanachama wapya zaidi ya 150 kutoka vyama vya ADC na ACT kujiunga na NLD na kupokelewa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Doyo Hassan Doyo.

отзывы реальных клиентов
Zaidi ya Bilioni 6 zaboresha miundombinu ya Elimu Muheza