Ukweli unaopaswa kuufahamu maishani
Ukweli ni uhalisia wa mambo, yaani jinsi kitu, hali au mahali kulivyo bila ya kuongeza kitu. Ni lengo laakili katika kujua mambo yote kwa dhati iwezekanayo. Ukweli pia unaweza kujulikana kuanzia hisia au kufikiria.
Lakini leo nataka nikuambie kweli ya mambo ambayo unapaswa kuifahamu hata kama nafsi yako inapinga lakini huo ndiyo uhalisia wa jambo lenyewe na ulipokee.
1.Kila msichana ni mrembo, inategemea tu ni Mvulana gani amemuona anafaa kuwa naye, yaani haramu kwako halali kwa mwingine.
2. Wakati mwingine kujenga umbali na watu huwa inasaidia kutambua ni kiasi gani una thamani kwao baada ya kupata habari au ukweli wa taarifa zao wananozizungumzia juu yako.
3. Mtu bora zaidi maishani mwako wa kwanza ni wewe mwenyewe, lakini wa pili ni yule anayekuja kwanza katika akili yako baada ya kusoma sentensi hii.
4. Zima au dhibiti hiosia zako kabla hazijakutawala, maana kuongozwa na hisia ni kubaya zaidi bali unapaswa kuwa na ziada katika maamuzi ambayo hayatakuingiza matatani.
5. Kwanza mara nyingi huwa inakuumiza, lakini kwanza hiyo hiyo hukubadilisha baadaye, hapa namaanisha hakuna mafanikio yanayokuja bila changamoto kwani ili uvune mahindi shambani utapanda na utapalilia pia.
6. Mtu anapokusaidia bila kulalama huo ni upendo, loakini yule anayekusaidia kisha akaanza kulalama au kutangaza muangalie mara mbilimbili maana anakudhalilisha.
7. Mtembea bure si mkaa bure, japo utulivu ni bora kuliko papara lakini kutulia sana ni kubaya kwani inahitajika uhangaike kwani mafanikio hayaji kwa kukaa bali kuhangaika.
8. Pambano ulilonalo leo ni kukuza nguvu zako za kesho, kwahiyo usiogope changamoto za maisha bali zikabili maana hakuna ushujaa pasipo na mapambano.
9. Usiwatendee watu ubaya kama wao walivyokutendea, watendee wema maana wema ni akiba na unapotendewa baya ukimya wako huwaumiza zaidi maana maisha ni “Mabadiliko” kupata ni majaliwa ya mola.
10. Marafiki wa uongo ni vivuli vyako visivyoweza kuonekana kwenye giza, kuwa makini na marafiki maana hata wahenga walisema kikulacho kinguoni mwako na mtu mbaya huwa hatoki mbali japo wanasema zimwi likujualo halikuli likakwisha.
11. Kila kitu kitafaa siku moja, penda klusikiliza kila kitu lakini chuja, hata pumba isikilize maana inawezekana maana ikakosa nafasi na pumba ikaja kukuokoa, Waswahili husema ganda la muwa la jana chungu kaona mavuno.
12. Baadhi ya watu wanaweza kukuchukia kwa sababu wanashindwa kukuangamiza, yaani wapo wato ambao hupenda tu kukuona ukiteseka ndiyo furaha yao bali ukifanikiwa ni chukizo kwao.
13. Hisia nzuri zaidi ulimwenguni ni kupendwa tena na mtu unayempenda, hata wahenga waliliona hili wakasema Mpende akupendaye kisha wakaongezea eti kofi la mpenzi haliumi.
14. Ili usimame, lazima ujue kuanguka chini, kuna usemi unasema ukupigao ndiyo ukufunzao na mtaka cha uvunguni ni sharti ainame, hivyo usiogope kuloana kama unahitaji kuvua samaki.
15. Usihukumu kamwe, penda kuthibitisha mwenyewe na si kwa wengine maana jambo la kusikia huwa limebeba fumbo ambalo ni mtego kwako, chunguza na thibitisha kabla.